Askari wa mgambo wa kijiji cha Ushokolo, Halmashauri ya wilaya ya kaliua mkoani Katavi wanatuhumiwa kumuua mkazi wa kijiji hicho, Juma Rajabu (40) kwa kutilopa sh 1000 ya mchango wa ujenzi wa choo cha shule ya msingi Ushokola.
Kwa mujibu wa gazeti la Uhuru, mkuu wa wilaya hiyo, Abeli Busalama amabye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama amesema tukio hilo limetokea siku ya jumanne saa 4 asubuhi.
Aidha amesema mgambo hao Moses Kiliano na Mganga Mparis wakiwa katika ukusanyaji wa mchango wa sh 1000 kwa kila familia kwaajili ya mchango wa ujenzi wa choo cha shule walitekeleza tukio la mauaji.
Ameongeza kuwa mgambo walipodai mchango katika familia ya marehemu ambapo walimkuta mke wa marehemu na alipowaambia kuwa hana wakamchukua hadi ofisi ya mtendaji wa serikali ya kjiji hicho kumsubiri mumewake kuja kulipa deni.
Busalama amebainisha bada ya Juma Rajabu kufika ofisini hapo alidaiwa kiasi hicho na kusema kuwa ameshalipa majibu ambayo walinzi hao hawakukubaliaana nayo hivyo wakaanza kumlazimisha alipe huku wakimpiga.
Amesema kuwa mara baada ya kuona wamemuumiza walimpeleka kituo cha polisi wilayani humo kwaajili ya kupewa PF3 na kumpeleka katika zahanati binasfi na kutokomea kusikojulikana lakini wakati juhudi za kumpatia matibabu hayo zikiendelea alifariki.