Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo ameziagiza familia zote jijini Dar es salaam kukaa kikao kujadili namna ya kukabiliana na ugonjwa wa COVID 19 na zikubaliane namna bora watayotumia kukabiliana na kirusi hiko kisichoonekana.
”Leo ninaomba kila familia katika Mkoa wa Dar es salaam ifanye kikao mkubaliane, kwenye nyumba mjadiliane kwenye familia katika ngazi ya familia, mmeamua kufa na corona au mnataka msife na corona na kama msife na corona mnachukua hatua gani ya kujilinda na ugonjwa huu” amesema Makonda.
Pia amekemea vikali tabia za baadhi ya wazazi ambao bado hawasikilizi wala kufuata maagizo ya Serikali iliyokemea mizunguko isiyo ya lazima amesema bado kuna baadhi ya wazazi wanakwenda club tabia ambayo ni hatari kwa watoto wao waliowaacha nyumbani kwani wanaweza kuwaletea kirusi hiko.
”Haiwezekani watu wazima shule zimefungwa, watoto wapo nyumbani, wewe unaenda usiku unakesha club halafu unarudfi unachekelea saivi hakuna kazi lakini nakula bata, unahatarisha maisha ya watoto wako unataka tuchukue bakora tukuchape yani unafika” Makonda.
Aidha Makonda amesema virusi hawa ni rahisi sana kukabiliana nao na kuwadhibiti kwa gharama ndogo ambayo ni tabia ya mtu ya mwenyewe, hivyo ameomba watanzania kusikiliza maagizo ya serikali kwani viongozi wamekuwa wakihangaika usiku namchana kufanya kila njia kuwakinga wananchi dhidi ya hili janga hivyoa meomba wachukue tahadhari na wajikinge na Corona.
Makonda ametoa agizo hilo kufuatia mwenendo mbaya wa ugonjwa wa Corona nchini, kwani hadi kufikia jana Aprili 17, 2020 kulikuwa na ongezeko la wagonjwa 53 na kufanya kuwa na jumla ya wagonjwa 147 na vifo 5.