Kiongozi wa ofisi ya rais wa Nigeria Muhammadu Buhari , Abba Kyari ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa katika utawala wa Rais huyo amefariki baada ya kupatikana na virusi vya Corona. 

Taarifa iliyotolewa kutoka ofisi ya raisa imesema kuwa marehemu alifariki jana Ijumaa kutokana na ugonjwa wa COVID-19.

Amefariki akiwa na umri wa takriban miaka 70, ni mtu wa kwanza mwenye cheo cha juu nchini Nigeria kufariki kutokana na ugonjwa wa COVID-19.

Nchi hiyo yenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika, imethibitisha visa 493 vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo 17.

Makonda: Barakoa ni lazima, ''ukate leso, ukate khanga''
Malawi: Mahakama yapinga kukaa ndani nchi nzima