Wizara ya afya nchini Ufaransa imesema wanajeshi wa majini 940 kati ya 2,300 waliokuwemo kwenye meli maarufu ya kivita ya kubeba ndege za kijeshi ya Ufaransa, Charles de Gaulle, wamekutwa na virusi vya Corona na kufanya meli hiyo kuegeshwa kwenye bandari ya Toulon.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa ” Kati yao wagonjwa 20 wamelazwa, 8 wanasaidiwa kupumua na mmoja yuko ICU”.
kwa mujibu wa taarifa hiyo, Jeshi limeanza uchunguzi ili kupata majibu yatakayowezesha kubaini corona imeingiaje kwenye meli hiyo.
Nchi hiyo hadi sasa ina takribani visa 149, 130 huku idadi ya waliofariki ikifikia 18, 703, waliopona ni 35,009 na kufanya nchi hiyo kushika nafasi ya nne kwa nchi zinazosumbuliwa zaidi na Corona.