Idadi ya visa vya wagonjwa wa covid 19 nchini Afrika kusini bado inaendelea kuongezeka, imefikia 3,034 baada ya visa 251 kuongezeka siku ya ijumaa.
Imeelezwa kuwa visa hivyo vimeongezeka kwa wingi baada ya serikali kuanza kufanya vipimo kwa wingi kwenye maeneo mbalimabali ya nchi.
Alipokuwa anatangaza visa hivyo, Waziri wa Afya nchini humo, Zweli Mkhize amesema watu zaidi ya laki moja wamepimwa na wengi ni kutoka ofisi binafsi.
Hata hivyo katika visa vya wagonjwa wa awali vimeongezeka vifo vya watu wawili na kufanya jumla ya vifo 52 kutokana na virusi vya Corona.
Waziri Mkhize ametoa onyo juu ya mazishi ya wanaokufa kwa corona na kusema “Tumegundua kuwa watu wanaohudhuria mazishi wanaambukizwa covid 19 kwasababu ya desturi zetu za mazishi”
Hata hivyo kati ya visa vyote vya wagonjwa ni wagonjwa 241 pekee ndio wapo hospitali na 36 wapo chini ya uangalizi maalum (ICU).