Baada ya video fupi iliyozunguka kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha Naibu waziri wa Afya, dkt. Faustine Ndugulile akisema barakoa za vitambaa hazizuii maambukizi ya corona, ameamua kutoa ufafanuzi juu ya hilo.

Jana kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika “Barakoa za kitambaa (cloth masks) hazina ubora wa kinga kama N-95 au surgical masks, lakini zinaweza kutumika kupunguza uwezekano wa maambukizi toka kwa mtu mmoja kwenda mwingine majumbani na sehemu za mikusanyiko. “

Amesema wakati wa kutumia barakoa hizo kuna mambo muhimu ya kuzingatia ambayo ni

1. Kutumia vitambaa vya pamba.

2. Kutumia layers zaidi ya mbili katika utengenezaji wa barakoa hizo.

3. Kuwa na barakoa angalau mbili ili kuruhusu kufanyiwa usafi wa mara kwa mara.

4. Barakoa zifuliwe kwa maji na sabuni na kupigwa pasi.

Lakini amesema ni muhimu kukumbuka kuwa barakoa si mbadala wa kunawa mikono na kuzingatia umbali kati ya mtu na mtu bali ni nyongeza ya hatua hizo.

Aidha amesisitiza kuwa kwa zile zinazotumika mara moja zinatakiwa zimchomwe moto, na watu hawapaswi kuazimana barakoa iliyotumika kila mtu anatakiwa kuwa na yake.

Vazi la kujikinga na Corona la Muhimbili kuokoa mamilioni ya fedha
Wachezaji Chelsea wakubali