Borussia Dortmund itamuongezea mshahara wa euro milioni 4 (£3.5m) winga wa Uingereza Jadon Sancho, 20, ikiwa atakataa ombi la kuhamia kwenye ligi ya primia. (Bild, via Mirror)

Newcastle huenda ikaonesha wazi nia yake ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Chile na mchezaji wa Barcelona Arturo Vidal, 32. Mchezaji huyo inasemekana kwamba yuko tayari kuhama ikiwapo timu ya The Magpies itabadilisha kocha wa sasa Steve Bruce na mahala pake kuchukuliwa na Max Allegri. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Beki wa Uhispania Pablo Mari, 26, anataka kufanya makubaliano yake ya uhamisho wa mkopo kwa Arsenal kutoka Flamengo kuwa wa kudumu msimu ujao. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa France Kylian Mbappe, 21, thamani yake itapungua hadi euro milioni 35 kutoka 40 baada ya virusi vya corona. (AS)

Arsenal na Everton ziko tayari kuingia kwenye vita ya kumsajili mshambuliaji wa Celtic raia wa Ufaransa Odsonne Edouard, 22. (Le10 Sport – in French)

Arsenal imewasiliana na Reims kwa sababu ya uhamisho wa mshambuliaji wa Ufaransa Axel Disasi, 22. (Goal)

Liverpool imeelekeza macho yake kwa kiungo wa kati wa Inter Milan na Croatia Marcelo Brozovic, 27. (Libero, via Mirror)

Hatahivyo, Liverpool haijawasiliana na RB Leipzig kuhusiana na uhamisho wa mshambuliaji wa Ujerumani, 24, Timo Werner. (General Anzeiger – in German)

Barcelona inataka kumuuza winga wa Brazil Philippe Coutinho – ambaye kwasasa yuko kwa mkopo Bayern Munich – kukiwa na matumiani kwamba kutapatikana mnunuzi anayemuhitaji mchezaji huyo, 27, kutoka ligi ya Primia. (Goal)

Liverpool itapunguza gharama ya winga wa Uswizi Xherdan Shaqiri, 28, kwasababu ya janga la virusi vya corona. (Football Insider)

Visa vya Corona Afrika Kusini ni zaidi ya 3,000
Gari latumbukia baharini laua watumishi watatu wa Bandari