Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, Tulia Ackson ametoa taarifa leo April 20, 2020 kuwa mbunge mmoja amepata maambukizi ya Covid 19 (Corona)
Akitoa taarifa hiyo katika kikao cha 12 cha Bunge mkutano wa 19, ameeleza kuwa Mbunge huyo alikwenda Jijini Dar es Salaam na alirudi jumatano iliyopita akaanza kujisikia vibaya.
Aidha Naibu Spika amewataka wabunge kuchukua tahadhari ya kujikinga na virusi hivyo kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na wizara ya afya mara kwa mara .
“Kwa mbunge anayeingia bungeni kukaa sehemu yake na siyo kuzunguka kwenye viti vya wengine,” amesema Tulia.
Katika hatua nyingine Naibu Spika ameeleza baada ya kikao kuhairishwa wabunge watatakiwa kuondoka maeneo ya bunge ili kutoa nafasi kwa ofisi na wataalamu wa afya kutakasa kwa dawa maeneo ya bunge.
Halikadhalika amewaonya wabunge kutoshirikiana vishikwambi (ipad) ama wengine wakitumia vipaza sauti vya wengine, jambo ambalo siyo sahihi kwa wakati huu wa corona.