Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia, wazee na watoto, katika taarifa yake iliyotolewa jana Aprili 20, imeeleza kuwa kuna ongezeko la vifo vya watu watatu waliothibitika kuwa na maambukizi ya covid 19.
Taarifa hiyo licha ya kueleza visa vipya vya waathirika wa corona 84 ambao 16 ni kutoka Zanznibar na wengine wote ni kutoka bara mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Pwani, Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Rukwa, Mtwara, Lindi, Manyara, Morogoro, Ruvuma, Mara na Kagera, imetaja ongezeko la vifo mkoa wa Dar es salaam.
“Tunasikitika kutangaza vifo vitatu (3), vilivyotokea jijini Dar es salaam, vya watu waliothibitishwa kuwa na maambukizi ya Covid 19, wizara inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, na Marehemu” Imeeleza taarifa hiyo.