Mmiliki wa nyumba moja katika mji wa Brooklyn nchini Marekani aliyefahamika kwa jina la Mario Selerno ameamua kufuta kodi ya nyumba ya mwezi wa nne kwa wapangaji wake takribani 200 kufuatia mlipuko wa janga la Corona lililopelekea watu zaidi ya milioni 10 nchini humo kupoteza ajira.
”Nimewaambia wasiwe na wasiwasi, wasipate taharuki, tunapitia katika kipindi kigumu na huu ugonjwa wa Corona, nitafuta kodi zote za mwezi wa nne”. amesema Mario.
Mario alipohojiwa amesema kuwa ameamua kufuta kodi ya mwezi huo sababu idadi kubwa ya wapangaji wake wamepoteza ajira zao hivyo anataka wawe na amani wahakikishe wana chakula cha kutosha japo wengi wao bado hawana uwezo hata wa kupata chakula.
”Nilisikia furaha na nimependezwa kufanya hivyo” amesema Mario..
Pia alipoulizwa kaisi gani amepoteza kufuatia kuwasamehe takribani wapangaji 200 aliowapangisha katika nyumba zake, Mario alijibu kuwa haukuwa wakati sahihi kujadili suala hilo kwani hawezi kufananisha thamani ya pesa na maisha ya binadamu.
”Najali sana maisha ya binadamu” Nimewaachia ujumbe mlangoni, Kaa salama, saidia jirani yako, na osha mikono yako” Mario.
Aidha, wapangaji wake wamemshukuru sana kwa uamuzi aliouchukua kwani amewasaidia sana kufuatia mlipuko wa janga la corona.