Meneja wa mshambuliaji wa timu ya Namungo FC, Ralient Lusajo ajulikanae kama Ahmed Kassim amesema mpaka sasa hajapokea ofa yoyote kuhusu nyota huyo.
Mshambuliaji huyo ambaye tayari amefunga mabao 11 mpaka sasa kwenye ligi kuu amekuwa akihusishwa kutaka kurejea kwenye timu yake ya zamani ya Young Africans aliyoichezea akiwa kijana mdogo.
Kassim hakuweka wazi mkataba wa mshambuliaji huyo umebaki muda gani ingawa amesema wanaipa nafasi ya kwanza Namungo FC katika mazungumzo kama watahitaji kuendelea kubaki na nyota huyo.
Meneja huyo ameongeza kuwa lolote linaweza kutokea ingawa hakupenda kuongelea sana suala la usajili wa nyota huyo ambaye ameonyesha uwezo mkubwa msimu huu.
“Mpaka sasa hakuna ofa yoyote rasmi kwa asjili ya Lusajo kinacho sikika ni tetesi tu. Katika mpira kila kitu kinawezekana ingawa kwenye mazungumzo tutawapa Numungo nafasi ya kwanza,” alisema Meneja, Kassim. Kassim ameamua kuweka sawa jambo hilo kufuatia baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kueleza kuwa, tayari klabu ya Young Africans imeshakamilisha taratibu za awali za usajili wa Ralient Lusajo.