Aliyekua nahodha na mshambuliaji Arsenal Robin Van Persie, amefichua siri ya kuachana na klabu hiyo yenye maskani yake makuu kaskazini mwa jijini London, na kutimkia Manchester United mwaka 2012.

Taarifa za awali zilieleza mshambuliaji huyo aliondoka Arsenal, baada ya kushindwa kuafikiana na uongozi wa juu kuhusu maslahi ya mkataba mpya, ambao alihitaji ufungamane na vipengele vya kusajiliwa wachezaji wenye hadhi ya kuipa mataji The Gunners.

Hii leo Van Parsie ambaye tayari ameshastaafu soka, amefichua siri na kueleza uvumi huo haukuwa kweli, kwani wakati huo alitamani kuendelea kuitumikia Arsenal ambayo ilimtazama kama mtetezi kwenye nafasi ya ushambuliaji.

Gwiji huyo kutoka nchini Uholanzi amesema taarifa zilizotolewa wakati ule zilikua kinyume chake, kwani viongozi wa Arsenal waligoma kumpatia mkataba mpya na ndio maana alifanya maamuzi ya kuondoka.

Amesema mpaka hii leo hakuna yoyote aliyekua nafahamu ukweli wowote, huku akitangaza dau kwa mdau yoyote mwenye ushahidi kama alikataa kusaini mkataba mpya ajitokeze na atamzawadia pesa.

”Kama kuna MTU atakuja na ushahidi juu ya Mimi kupewa mkataba mpya nampa pesa ”

“Sikuwa na maelewano na mtendaji mkuu kwa wakati huo Ivan Gazdiz, na ndio maana niliamua kuondoka, suala la mimi kuweka masharti makubwa kwenye mkataba mpya halikuwepo.” alisema Van Persie.

Van Persie alisajiliwa na Manchester United chini ya utawala wa Sir Alex Ferguson kwa dau la Paundi milioni 24.

Akiwa na klabu hiyo Van Persie alifanikiwa kutwaa taji la England katika msimu wake wa kwanza (2012–13), na baadae akaongeza taji la ngao ya jamii (FA Community Shield) mwaka 2013.

Hadi anaondoka Arsenal mwaka 2012, Van Parsie alikua amefunga mabao 96 katika michezo 194 aliyocheza, na kwa upande wa Manchester United alicheza michezo 86 na kufunga mabao 48.

CORONA: Mashabiki washauri Ozil apigwe bei
Soko la SADC kushindana ubora wa bidhaa