Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania na mwenyekiti wa kamati ya kiufundi ya Mashirika ya Viwango ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya kiuchumi kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt Athuman Ngenya amewataka wazalishaji wa bidhaa mbalimbali kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kushindana katika soko la SADC.

Dkt, Ngenya ametoa wito huo mapema leo wakati wa mkutano wa 42 wa kamati ya kiufundi ya mashirika ya viwango ya nchi wanachama wa SADC unaofanyika kwa njia ya mtandao katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Dkt .Ngenya amesema mbali na mkutano huo kujadili masuala ya viwango na kanuni zake pia unajadili kuondoa vikwazo vya kibiashara vinavyokwamisha maendeleo ya biashara katika nchi wanachama pamoja na umuhimu wa kuwa na sera ya ubora kwa nchi za Afrika ambayo rasimu yake imekwishaandaliwa.

Mkutano huu wa 42 ambao mwenyeji ni Tanzania kauli mbiu ni ” matumizi ya viwango na kanuni ni kukuza ushindani na masoko ya wajasiriamali.

Van Persie afichua kilichomuondoa Arsenal
Muhimbili yasambaza mavazi ya kukinga Corona wauguzi