Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu Bungeni jijini Dodoma amejibu malalamiko mbalimbali kuhusu takwimu zinatolewa za visa vya corona nchini kuwa si za sahihi.
Ummy amekanusha na kusema kuwa taarifa zinazotolewa ni sahihi na hakuna usiri kwani takwimu zinatolewa kadri zinavyopatikana maabara.
”Tungekuwa tunaficha takwimu za corona tusingetoa takwimu zinazoonesha Tanzania tuna wagonjwa wengi kuliko nchi nyingine Afrika Mashariki, tusingetoa hizo takwimu, kwahiyo wameniambia hakuna usiri tunatoa takwimu, kadri tunavyozipata maabara lakini wataalamu wameniambia hakuna haja ya kutoa taarifa kila siku” Amesema Ummy.
Pia amesema kuwa Shirika la Afya Duniani lilitoa agizo moja tu lililowataka kila nchi kutangaza kisa cha kwanza cha Corona ambapo kwa Tanzania kilitangazwa kile cha Isabela ambae alikuwa mkazi wa Arusha ambaye alipata maambukizi nje ya chi alikokuwa kwenye shughuli zake.
”Obligation ya kwanza ya WHO ilikuwa ni kutoa taarifa ya kwanza ya kwamba tumetoa case ya covid 19 Tanzania tumefanya, kwahiyo hizo tunakaa tunazichambua tunatoa taarifa kwahiyo hakuna haja ya kuwa na usiri” Ameongezea Ummy.
Aidha, Waziri Ummy mwalimu amewataka watanzania kuendelea kuchukua tahadhari juu ya virusi vya Corona na kufuata taratibu zote zinazotolewa na wataalamu kujikinga na ugonjwa huo wa COVID 19.
Hadi sasa Tanzania ina jumla ya visa 480 kutoka mikoa mbalimbali, Keya kukiwa na Visa 396 na Uganda Visa 83.