Rais wa Marekani, Donald Trump ameendela kushikilia msimamo wake kwamba virusi vya corona chimbuko lake ni katika maabara ya utafiti ya nchini China kwenye mji wa Wuhan.
Amegongelea msumari ajenda hiyo wakati akijibu swali la mwandishi wa habari katika Ikulu ya White House huko Washington.
Amesema kwamba serikali ya China ilishindwa kudhibiti kirusi hicho nchini mwake, matokeo yake ulimwengu sasa unateseka vibaya sana.
Trump pia ametoa kitisho kuwa anaweza kuiongezea ushuru China iwe kama adhabu kwao.
Aidha kumekuewa na tetesi kuwa huenda mlipuko wa janga la ugonjwa wa COVID-19 Marekani, linatishia nafasi ya Trump ya kuchaguliwa tena katika uchaguzi wa mwezi Novemba.