Jeshi la Polisi mkoani Mtwara linawashikilia watu watatu wakiwemo watumishi wawili wa hospitali ya wilaya ya Tandahimba mkoani humo kwa tuhuma za kuiba Utra Sound ya hospitali hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara ACP Mark Njera amesema kuwa tukio hilo limetokea Aprili 23 mwaka huu katika hospitali ya wilaya ya Tandahimba

Ambapo daktari anayefahamika kwa jina la Yuves Katambi alimshawishi mwendeshaji wa mashine hiyo Abasi Katambi wote madaktari wa hospitali hiyo kuiba Ultra sound yenye thamani ya shilingi milioni kumi na nne na laki tano.

ACP Njira amesema walifanikiwa kuiiba majira ya saa mbili usiku kwa kuvunja ofisi na kwenda kuificha kwa bwana Sauli Mkomagi mkazi wa Kijiji cha Nangamba mkoani humo.

ATCL yaanza kusafirisha mizigo nje ya Nchi kukabili Corona
Trump ashikilia msimamo: Corona imetoka maabala ya China