Mwanafuzi mwenye umri wa miaka (9) darasa la tatu katika shule ya msingi Likuyuseka wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma Jeska Kifaru anaomba wasamalia wema kumsaidia mchango wa fedha ili aweze kupata matibabu ya moyo katika hospitali ya Muhimbili.
Kwa mujibu wa Gazeti la Majira Jeska amesema anaomba msaada baada ya wazazi wake kushindwa kumpeleka kupata matibabu kutokana na kipato duni.
Naye mama mzazi wa mwananfunzi huyo Stamili Abdallah Gehu amesema, wanaendelea kutumia dawa kutoka katika hospitali ya Peramiho japokuwa hali ya binti yao inaendelea kuwa mbaya kwani amekuwa akibadilika rangi na kuwa mweusi baada ya rangi yake ile ya awali kuanza kutoweka kila kukicha.
Ameongezea kuwa walifika ofisi za mkuu wa wilaya ya Namtumbo kuomba kibali cha kuomba kuchangisha fedha ili waweze kumpeleka binti yao hospitali.
Aidha, mwalimu mkuu wa shule ya msingi Likuyuseka, Bonifasi Sichele amesema kabla ya corona, mwanafunzi wake Jeska alikuwa anahudhuria shule na kuipenda licha ya kuwa mdhaifu na kutoonyesha furaha mara kwa mara darasani kwa kusumbuliwa na moyo lakini anafanya vyema katika masomo yake.
kuisaidia familia yake wasiliana nao kwa namba za simu ya mkononi 0715490997 ili waweze kumpeleka mtoto wao hospitali ya Taifa Muhimbili.