Mchungaji Dkt. Peter Mitimingi amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Mei 4, 2020.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mchungaji ambaye alikuwa msaidizi wake, Mchungaji Samweli amesema ni kufuatia sukari kupanda na kisha Mitimingi alipata homa ya mapafu kutokana na baridi iliyokuwepo Arusha.
”Yeye alikuwa anaumwa Sukari ilipanda, ikaanza homa ya mapafu kwasababu alikuwa Arusha akapigwa na mvua kukawa na baridi kali hiyo hali ikamsumbua na kupelekea kufariki “-Mchungaji Samweli, Msaidizi wa Kanisa.
Aidha Mchungaji Mitimingi alipata umaarufu mkubwa kupitia mafunzo yake juu ya mahusiano ambayo watu wengi walikuwa wanayatumia.
Marehemu Mitimingi alikuwa kiongozi wa Kanisa la Warehouse Christian Center(WHC)
Na pia alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma ya the Voice of Hope Ministry, Mshauri wa Saikolojia wa BLCCC.