Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga amemaliza bifu lililokuwepo kati ya chombo hicho cha habari na msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na kuamuru nyimbo zake zianze kupigwa mara moja na media hiyo.
Kusaga amesema hayo wakati akizindua kampeni ya BONGE LA MPAMBANAJI ambayo ni maalum kwa ajili ya kuwawezesha Wahudumu wa Afya Tanzania kwa vifaa tiba na mahitaji mengine kwenye vita hii dhidi ya kirusi cha corona.
Kusaga kupitia kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM , amesema anao wapambanaji wenzake ambao wako tayari kuungana na yeye na miongoni mwao ni Diamond Platnumz ambaye alimpigia simu LIVE na kuzungumza kwenye kipindi.
Akiongea kwenye PB Diamond amesema; “Kwanza nimpongeze CEO Kusaga kwa kuweka nguvu zake kwenye hilo sio kila Mtu mwenye moyo huo, mimi pia nitaweka mchango wangu hapo na kama unavyofahamu tayari pia upande wangu nimeanza kulipia kodi familia zilizokwama kutokana na hii corona”
Baada ya kuzungumzia Bonge la Mpambanaji, CEO Kusaga alimtaka Diamond achague wimbo wake ili uchezwe kwenye PB kuwaamsha Wapambanaji wote ambapo mara ya kwanza alipendekeza apigwe Msanii wake mpya @officialzuchu lakini baada ya Jo kusisitiza kuwa ngoma ya Diamond ndiyo inatakiwa, Platnumz alichagua yope remix na ikapigwa.