Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Mkoa wa Geita, Hamim Buzohera Gwiyama amefariki leo may 6, 2020 asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Waziri wa Nchi – TAMISEMI, Selemani Jafo ametoa pole wa familia na ndugu na kueleza taarifa zaidi kuhusu mazishi zitatolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita.

Marehemu aliteuliwa na Rais Magufuli Juni 26, 2016 kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale ambapo kabla aliwahi kufanya kazi sehemu mbalimbali.

RC Chalamila atamani wabunge wachapwe viboko
Rais Magufuli amkosha Laila Ali