Kwa mara ya kwanza katika maisha yake, mwanzilishi wa programu mpya ya mawasiliano Zoom , Eric Yuan aliorodheshwa katika orodha ya Forbes ya mabilionea akiwa na mali yenye thamani $ 7.8 billion .
Yuan ameeleza kuwa wazo la kuanzisha zoom lilimjia alipokuwa mwanafunzi wa chuo ambapo alilazimika kupanda treni kilasiku kwenda kumtembelea mchumba wake jambo lililomkera.
“Mara ya kwanza nilipofikiria kuhusu Zoom , ni wakati nilipokuwa mwanafunzi wa Chuo kikuu nchini China na nilikua nikipanda treni kila siku kwenda kumuona mchumba wangu ambaye sasa ni mke wangu”, alisema Yuan
Ameongeza kuwa “Nilikerwa na safari hizo za mara kwa mara na nikaanza kufikiria njia nyengine za kumtembelea mchumba wangu bila ya kusafiri…Ndoto hizo hatimaye zilitimia na kuwa kampuni ya Zoom Foundation”
China yaripoti visa vipya vya Corona
Mwana huyo wa muhandisi , Yuan alizaliwa katiika mkoa wa Shandong nchini China. Baada ya kusomea uhandisi chini China , alielekea kufanya kazi nchini Japan kwa miaka minne kabla ya kununua tiketi ya ndege kuelekea Marekani.
Alianza kufanya kazi kama msimamizi wa programu katika kampuni ya Wev Ex. Miaka kumi baadaye kampuni hiyo ilinunuliwa na Cisco Systems , ambapo Yuan alipanda ngazi na kuwa makamu wa rais wa uhandisi katika kampuni hiyo.
Mwaka 2011, muhandisi huyo aliwasilisha mradi wake wa kuvumbua programu ya mawasiliano ambayo itafanyakazi katika tarakilishi na pakatalishi na pia katika simu.
Wazo hilo lilikataliwa na Yuan akajiuzulu katika kampuni hiyo ili kuanzisha biashara yake ya Zoom.
Baada ya kujiuzulu katika kampuni ya Cisco , ilikuwa vigumu kupata wawekezaji ambao waliamini mradi wake.
Alilazimika kuomba fedha kutoka kwa marafiki na watu wa familia ambao waliamini mradi wake kulingana na gazeti la Financial Times.
Ameeleza kwamba upanuzi wa simu aina ya smartphone na teknolojia ya kuhifadhi ulitoa mazingira ya Zoom kuwanzishwa.
Mwishoni wa mwaka uliopita mambo yalianza kwenda vyema , lakini hali ikabadilika ghafla wakati mlipuko wa virusi vya corona ulipoanza kusambaa kote duniani.
Katikati ya mlipuko huo, masoko ya kifedha yalishuka huku hisa za Zoom zikipanda hadi asilimia 14 mwaka huu.
Mwezi Disemba kampuni hiyo ilikuwa na wateja milioni 10 kwa siku na ilipofikia mwezi Machi ilikuwa na wateja milioni 200 na kufikia mwezi Aprili wateja waliongeza hadi milioni 300 kulingana na data yake.
Wataalam wa teknolojia wanakubaliana kwamba ukubwa wa bidhaa unatokana na sababu ya kwamba bidhaa hiyo ni rahisi kuitumia , na haimuhitaji mtumiaji kujisajili , na hadi watu 100 wanaweza kujiunga katika mawasiliano na kwamba ni bure kwa simu hadi dakika 40.