Mpaka wa Tanzania na Zambia, (Nakonde), umefungwa rasmi leo Mei 11, 2020 baada ya nchi ya Zambia kurekodi visa vingi vya corona ndani ya siku moja jumapili ya jana.
Katika visa hivyo 85 na vifo vitatu ndani ya siku moja visa 76 vimeripotiwa kutoka katika mpaka Nakonde uliopo mjini Tunduma baada ya kupima watu 250.
Waziri wa afya nchini Zambia, Chitalu Chilufya amesema wamefunga mpaka huo kuanzia leo kwa muda ambao bado haujajulikana.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, rais wa nchi hiyo, Edigar Lungu alitangaza kufungua baadi ya biashara ambazo zilifungwa Mach18 kuzuia maambukizi ya corona, kama sehemu za mazoezi, na starehe za usiku kwa kusema kuwa uchumi umezorota.
Hadi sasa nchi ya Zambia imethibitisha visa 267 vya wagonjwa wa corona waliopona 117 na vifo 7.