Mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani na Mbunge wa Bunda mjini (Chadema), Easter Bulaya amejibu tuhuma za Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali alizotoa jana, wakati anatangaza kuhama chadema kwasababu ya manyanyaso.

Bulaya amesema kuwa Mbunge huyo alipaswa kuweka akiba ya maneno na kuhama chama kwa ustaarabu kwani kuhama vyama ni jambo la kawaida.

Amesema utaratibu wa kuchangia chama ili kukijenga ulipitishwa na kamati kuu ambayo wabunge ni wajumbe ambao waliamua kuhakikisha chama kinajengwa na nguvu zao.

” Sisi tuliamua wenyewe na wabunge ni wajumbe wa baraza kuu wakasema no, tunataka chama chetu tukijenge tusitegemee ruzuku pekeyake michango ipo kikatiba” Amesema Bulaya

Balozi wa Kenya aomba Corona isiharibu mahusiano na Tanzania

Pia ametolea ufafanuzi jibu alilojibiwa Lijualikali kuwa uchaguzi ni mchakato baada ya kuuliza hela za michango zimeenda wapi “uchaguzi sio ile tarehe ya kupiga kura uchaguzi ni maandalizi ya uchaguzi”.

Aidha amesema kuwa Wabunge kuhama chama hicho hakuyumbishi harakati za chama kwani wao wanaamini juu ya nguvu ya wanachama wao ambao ni zaidi ya milioni 10.

Marekani kusitisha ufadhili WHO ndani ya siku 30 zijazo
Kisongo: Ndemla hana washauri wazuri