Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ametangaza visa vipya vya Corona ambavyo vimethibitishwa katika mpaka wa Namanga vya madereva 21 wa malori kutoka Kenya na mmoja kutoka Uganda.

Gambo amesema kufuatia ongezeko la visa vya Corona mipakani, mkoa huo umeanzisha utaratibu wa kuwapima madereva wa malori wanaotokea Kenya kupitia Namanga.

Sampuli zilichukuliwa tarehe 14,16 na 18 ya mwezi Mei ambapo madereva 44 walipimwa Mei 14 na iligundulika 14 wana maambukizi na 30 wapo salama. Kati ya madereva hao 14, 11 ni raia wa Kenya, 1 ni kutoka Uganda na uraia wa madereva wengine wawili umehifadhiwa.

Majibu ya sampuli 23 za Mei 16 yalithibitisha madereva 10 wote Wakenya wana covid -19 na wengine 13 walikutwa hawana. Sampuli za Mei 18 bado zinaendelea kufanyiwa vipimo na majibu yatatolewa yakishapatikana.

Corona kutozuia chanjo kwa watoto
CAS kumaliza utata Juni 08-10