Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), imesema kuwa rufaa ya klabu ya mabingwa wa soka nchini England Manchester City, itasikilizwa Juni 8 hadi 10 na kutoa hukumu.

Manchester City waliwasilisha rufaa mahakamani hapo kupinga adhabu iliyotolewa na Shirikisho la soka Barani Ulaya (UEFA), baada ya kukutwa na kosa la kukiuka kanuni za matumizi ya kiwango cha pesa katika kusajili wachezaji.

Timu zote ulaya zimewekewa kiwango cha juu wanachoruhusiwa kutumia katika kusajili ili kuzipa nafasi sawa timu zisizo tajiri kuweza kushindana kwa usawa ingawa hazina utajiri wa kutisha.

Kama klabu hiyo itaendelea kuthibitika ina kosa la kukiuka kanuni za matumizi ya kiwango cha pesa za usajili, haitoshiriki michuano hiyo kwa muda wa miaka miwili na nafasi yao itachukuliwa na timu itakayomaliza nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu England.

Adhabu ya awali inaifanya Manchester City kutoshiriki michuano ya ligi ya Mabingwa Barani Ulaya (European Champion League) na Europa League katika misimu ya 2020 / 2021 na 2021/ 2022. Adhabu hiyo iliendana na faini ya Euro 20,000,000.

Madereva 21 Wakenya wakutwa na Corona, mpaka wa Namanga
Uchaguzi Mkuu Burundi leo, baada ya Nkurunziza kuongoza miaka 15