Baada ya vuguvugu la wakulima wa Pamba wilayani Maswa mkoani Simiyu kudhulumiwa fedha zao na viongozi wa vyama, imeelezwa kuwa fedha hizo zimeanza kurejeshwa.
Viongozi hao wa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) wanadaiwa kutafuna shilingi milioni 232 za wakulima katika msimu wa kilimo wa mwaka 2019 – 2020.
Imeelezwa kuwa waliteketeza fedha hizo kutokana na kuzitumia kwa kuchezea mchezo wa upatu na kukopeshana.
Viongozi hao wameanza kurejesha fedha baada ya kukamatwa na jeshi la polisi na kufikishwa katika Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) katika wilaya hiyo.