Baada ya mlipuko wa 11 wa Ebola kutangazwa wiki iliyopita, wahudumu wa afya kaskazini magharibi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameanza kutoa chanjo.
Watu sita wamefariki kutokana na virusi hivyo hatari tangu Juni mosi, wakati visa vya kwanza viliporipotiwa Mbandaka, mji mkuu wa mkoa wa Equateur.
Waziri wa Afya Eteni Longondo ameliambia shirika la habari kutoka Mbandaka kuwa zoezi la utoaji chanjo lilianza Ijumaa, na tayari wahudumu wa afya wameshapata chanjo hiyo, pamoja na watu waliokuwa karibu na visa vilivyothibitishwa vya maambukizi.
Amesema wana dozi 1,500 na wameagiza nyingine 8,000 zaidi ili kuwahudumia watu wengi wa Mbandaka. ambapo zaidi ya watu 300,000 tayari wamepewa chanjo ya Ebola katika mlipuko uliotokea mashariki mwa nchi hiyo.