Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta tayari wametangaza bendera za nchi zao kuwekwa nusu mlingoti kuomboleza kifo cha Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza huku bendereza za makao makuu ya EAC nazo zikiwa nusu mlingoti tangu kilipotangazwa kifo cha Rais huyo.

Magufuli ametangaza maombolezo ya Kitaifa ya siku 3, (kuanzia Juni 13 hadi Juni 15) kwa kuesema Tanzania imetoa heshima hiyo kwa kutambua kuwa Rais Nkurunziza alikuwa Rais wa nchini jirani ambayo imekuwa na uhusiano na ushirikiano mzuri wa kirafiki, kihistoria, na kindugu na Tanzania.

Rais Magufuli amesema “Burundi ni mwanachama mwenzetu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Rais Nkurunziza aliipenda Jumuiya hii, pia aliipenda Tanzania na alishirikiana nasi kila ilipohitajika”.

Rais Nkurunziza alifariki Juni 9 katika hospitali ya Karusi Fiftieth Anniversary baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo Juni 8, Serikali ya Burundi imetangaza maombolezo ya siku 7, na bendera yao itapepea nusu mlingoti kwa siku zote hizo.

Msajili ampa Zitto siku saba, Kikao na Balozi wa Uingereza champonza
Mkude hadi mwishoni mwa mwezi