Waziri wa Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Selemani Jafo ametoa agizo kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano kuripoti shuleni ndani ya wiki mbili na wasipofanya hivyo nafasi zao zitachukuliwa.
Amebainisha hayo leo, baada ya Rais Magufuli kutangaza shule zote kufunguliwa kuanzia June 29 na Waziri wa Elimu Prof, Joyce Ndalichako kutangaza ratiba ya masomo na mitihani.
“wale wanafunzi wa form 5 ambao hawataripoti kwa wiki mbili nafasi zao zinachukuliwa na wanafunzi wengine na ambaye hatadhibitisha nafasi yake kwa wakati nafasi yake itachukuliwa. Hatutaki kusikia malalamiko mara baada ya maelezo tunayoyatoa”. Amesema Waziri Jafo
Kwa upande wa Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako amesema Utaratibu wa kidato cha tano wapya kuanza masomo utatolewa na waliopo watasoma na kukamilisha masomo ya kidato cha tano na kufanya mitihani July 24 na July 27 wataanza masomo ya kidato cha sita.