Klabu ya Leicester City ipo vitani kuwania saini ya mlinzi wa kati wa Burnley na England James Tarkowski, pia mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 27 anawindwa na klabu ya Crystal Palace.
- Dili la mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner 24, kwenda kujiunga na miamba ya England Chelsea litakamilika wiki hii, ambapo tayari timu hizo mbili zimekubaliana dau la £53.
- Juventus wanahitaji kumsajili kiungo mkabaji wa Chelsea na Italia Jorginho, 28, sambamba na beki wa kushoto wa timu hiyo Marcos Alonso, 29.
- Manchester City wanaangalia uwezekano wa kumsajili beki wa Morocco na Real Madrid ambaye anakipiga kunako klabu ya Borrusia Dortmund ya Ujerumani Achraf Hakimi.
- Kiungo wa zamani wa Uholanzi Ronald de Boer amesema kiungo wa Ajax ambaye anawindwa na vilabu vya Manchester United na Real Madrid Donny Van de Beek, 23, ni heri aende Madrid kuliko United.
- Meneja wa Tottenham Jose Mourinho anahitaji kumsajili mlinzi anayemaliza muda wake ndani ya Paris St-Germain Thiago Silva, 35, bure mwishoni mwa msimu huu.
- Arsenal imeripotiwa ipo tayari kumpa mshahara mara tatu wa ule anaopokea Atletico Madrid kiungo mkabaji wa Ghana na Atletico Thomas Partey, 27, ili ajiunge na timu hiyo.
- Norwich wako hatua za mwisho kukamilisha uhamisho wa kinda wa Sunderland Bali Mumba, 18.