Burundi imemuapisha rais mpya wa taifa hilo, Evariste Ndayishimiye, katika hafla iliofanyika mbele ya raia wa taifa hilo na baadhi ya viongozi kutoka mataifa tofauti.
Everiste Ndayishimye aliibuka mshindi baada ya uchaguzi uliofanyika Mei mwaka huu Kwa mujibu wa Tume ya uchaguzi ya Burundi.
Katika kiapo chake rais huyo ameapa kulinda katiba ya Burundi, kuheshimu umoja wa raia wa taifa hilo, kutoa haki kwa wote mbali na kutetea mipaka ya taifa hilo.
Sherehe hiyo iliofanyika katika uwanja wa kandanda wa Ingoma katika mkoa wa Gitega imefanyika wakati ambapo taifa hilo limeathirika na mlipuko wa vurusi vya corona.
Rais Evariste baada ya kumaliza kula kiapo alikagua gwaride la kijeshi na baadaye kutoa hotuba .
Aidha hayo yamejiri baada ya aliyekuwa rais nchini humo, Piere Nkurunzinza kuaga dunia kwa kisa kilichotajwa kuwa ni mshtuko wa moyo uliopelekea kuaga dunia.
Aidha Nkurunzinza amekuwa kiongozi wa taifa hilo kwa takribani maika 15.
Ndayishimiye ni mwanasiasa wa karibu wa Nkurunziza na amekuwa Katibu Mkuu wa Chama tawala cha CNDD-FDD tangu mwaka 2016.