Rais wa zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein ametangaza rasmi kufunguwa kwa shule zote visiwani humo pamoja na shughuli za kijamii kuanzia Juni 29 baada ya kupungua kwa kasi ya maambukizi ya virusi vya Corona.
Amebainisha hayo wakati akizungumza katika hotuba ya kulivunja Baraza la Wawakilishi la 9 huko Chukwani na kusisitiza kuwa hatua hiyo inapaswa kwenda sambamba na tahadhari kubwa ya kuendelea kujikinga.
Aidha ameiagiza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuaandaa mpango utakaozingatia kukabiliana na wimbi kubwa la Wanafunzi pamoja na vifaa vya skuli ili kuepusha kuenea kwa kasi kwa maradhi hayo.