Rais wa awamu ya saba Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein ameaga baraza la wawakilishi na kulivunja huku akijivunia mafanikio aliyoyapata katika utawawala wake wa miaka 10 visiwani humo hususan sekta ya uchumi.
Amesema Serikali yake iliweza kuongeza ukusanyaji wa mapato, kuimarisha nidhamu ya matumizi, kupunguza utegemezi wa wafadhili na kujiepusha na misamaha ya kodi.
Huku pato la Zanzibar likiongeza kutoka Sh. 1,768 bilioni mwaka 2010 hadi kufikia bilioni 3,508 2019/20 ikiwa ni ongezeko mara 1.74 tangu alipoingia madarakani.
Amesema uchumi wa zanzibar umekuwa kutoka asilimia 4.3 mwaka 2010 hadi asilimia saba 2019/20, huku kipato cha wananchi kikiongezeka kutoka sh. 942,000 hadi milioni 2 kwa mwaka na ongezeko la asilimoa 170.59.
Aidha amesema miongoni mwa mafanikio mengine aliyoyapata ni kulinda amani, utulivu na mshikamano wa wazanzibar.
“Pamoja na majukumu ya kuwatumikia wananchi na kujibu malalamiko ya wananchi wa Zanzibar katika kipindi chetu madarakani, tusingeweza kufanikiwa bila kulinda amani, usalama na umoja” Amesisitiza Dkt. Shein