Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa kuteuliwa, Prof. Palamagamba Kabudi ametangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Kilosa mkoani Morogoro.
Ametangaza ni hiyo jana kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi wa handaki lenye urefu wa km. 1.1 pamoja na jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Rudewa – Kilosa yenye urefu wa km. 24 uliofanywa na Rais John Magufuli.
Kabudi aliwaambia wananchi wa Kilosa kuwa yey ni mzaliwa wa Kilisa na wazazi wake asili yao ni wilayani humo, kauli iliyofanya ashangiliwe na wananchi hao.
“Na mimi ni mtoto wenu ikimpendeza Mungu, na nikapata kibali, sikatai kuwa mtumishi wenu” alisema Kabudi.
Aidha alimuomba rais afikirie Kilosa kuhusu ujenzi wa reli ya Kilosa – Mikumi – Kidatu hadi Mlimba na kusaidia kuunganisha Kilosa na bonde la Kilombero.