Serikali ya Uingereza imetunga sheria inayowabana watu wasiovaa barakoa wanapoenda kufanya manunuzi kwenye maduka mbalimbali, kwa kuwapiga faini ya £100 (Sawa na Sh. 263,000 za Tanzania).
Kiwango hicho cha faini kwa mtu aliyekaidi amri hiyo kinapaswa kulipwa moja kwa moja kwa polisi.
Hata hivyo, Serikali imewataka wanaotoa huduma kwenye maeneo ya kufanya manunuzi kuwashauri tu wateja wao kuvaa barakoa lakini hawapaswi kuchukua hatua yoyote dhidi yao.
Wasiopaswa kuvaa barakoa ni wale tu wenye ulemavu wa aina inayowasababisha wasivae barakoa pamoja na watoto wadogo. Amri hiyo inaanza kufanya kazi rasmi Julai 24, 2020.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amesisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu sana kwakuwa itawalinda watu wengi zaidi dhidi ya virusi vya corona, na kwamba uvaaji wa barakoa katika maeneo ya umma itakuwa sio jambo la hiari tena.
Hatua hiyo ya Serikali ya Johnson imepata pingamizi kutoka kwa wakosoaji wake ambao wanadai kuwa ni vyema zaidi kuamini katika utashi wa watu badala ya kuwalazimisha kuvaa barakoa.
Nchini Uingereza pekee, watu zaidi ya 290,000 wamethibitika kupata virusi vya corona (covid-19), na watu 44,830 wamepoteza maisha kutokana na virusi hivyo. Kwa bahati mbaya hakuna hata mgonjwa mmoja aliyepona hadi sasa.
Bill Gates aeleza dawa ya corona inavyopaswa kusambazwa
Mgonjwa wa kwanza wa corona aidai Serikali ‘mamilioni’ – Kenya