Msanii nguli wa R&B Nchini Marekani Robert Kelly anayekabiliwa na kesi ya unyayasaji wa kijinsia pamoja na watu wa tatu wamekamatwa na kushtakiwa kutokana na kuhusika kujaribu kuwapa rushwa na kuwatishia maisha wanawake waliomstaki msanii huyo.
Kwa mujibu wa NBC News-New York, watu hao wanaohisiwa kuwa na ukaribu na Mwanamuziki huyo walijaribu kutega kitu chenye asili ya bomu katika gari la baba wa mmoja wa wanawake waliomshtaki R. Kelly.
Lamar Odom ajutia kuukataa ushauri wa Jay-Z
Shtaka hilo lililofunguliwa na mwanasheria wa wanawake hao, limewataja watu hao kuwa ni Richard Airlines, Donnell Russell na Michael Williams ambao wote wana uhusiano wa karibu na mwanamuziki huyo
Licha ya ushahidi mkubwa kuthibitisha kuwa R.Kelly alihusika katika unyanyasaji wa kijinsia, lakini ameendelea kukana mashtaka yote yanayomkabili.