Mahakama nchini New Zealand imetangaza hukumu dhidi ya aliyekua mtuhumiwa wa mauaji ya kigaidi ya Christchurch, Brenton Tarrant, baada ya kusikiliza kesi ya kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Tarrant alishambulia msikiti wa Nur na Linwood kwa silaha huko Christchurch wakati wa sala ya Ijumaa mnamo Machi 15 mwaka 2019, ambapo watu 51 walipoteza maisha (mmoja wao aliakua raia wa Uturuki), na wengine 49 walijeruhiwa (Wakiwemo Waturuki wawili).
Hukumu ya Tarrant imetolewa kwa sharti la kifungo hicho kutokuwa na uwezekano wa kupunguzwa, kwani makosa aliofanya ni ukatili wa kiwango kikubwa, nab ado imechukuliwa hukumu ya maisha jela haiwezi kufuta hasara na maumivu alioisababishia jamii.
Jaji Cameron Mander amesema hukumu hiyo, ndiyo ya juu zaidi kutolewa nchini New Zealand na imelenga kuonesha jinsi matendo ya Tarrant yalivyokosa utu na ubinadamu.