Moto mkali katika bandari ya Beirut umesababisha hofu kubwa katika mji mkuu wa Lebanon ,siku mbili tu baada ya moto mwingine kuzimwa eneo la mlipuko mkubwa ulioua karibu watu 200 mwezi uliopita .
Jeshi la polisi Lebanon limesema moto huo ulilipuka kwanye ghala la kuhifadhi mafuta na matairi katika eneo la Ushuru wa bandari
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema waliona watu wakikimbia kuelekea upande wa pili wa moto , ambao ulipeleka moshi mkubwa angani .pia aliona magari yakibadili uelekeo katika kotongoji cha Mar mikhael ambacho kiliharibiwa na mlipuko wa Agosti 4 na kujeruhi zaidi ya watu 6,500 na kuwaacha mamia ya watu bila makazi .
Chanzo cha usalama kimeviambia vyombo vya habari kuwa moto huo ulitokea katika eneo la kuhifadhia mvitu mbalimbali na linalotumiwa na usafirishaji wa BCC .
Wakati wa kuzuka moto ,kazi ilikuwa ikifanywa ili kuondoa bidhaa zilizoifadhiwa katika maghala yalioharibiwa na kazi ya ujenzi zilikuwa zikiendelea .