Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imekanusha kuinyima kibali helikopta ya mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu iliyokuwa itumike katika mikutano yake ya kampeni kuelekea Uchaguzi mkuu.

Taarifa rasmi iliyotolewa na mamlaka hiyo, imesema helikopta hiyo imepewa kibali cha muda mrefu (block permit) na TCAA kwa shughuli za kampeni za uchaguzi kuanzia Septemba 4 hadi Oktoba 31, 2020.
 
Mkurugenzi Mkuu TCAA, Hamza Johari amekanusha pia uwepo wa ofisa wa mamlaka hiyo aliyetoa taarifa kuhusu safari ya msafara wa Lissu  kutokuwepo kwani safari ya CHADEMA haikuwepo kwenye orodha. 

Ufafanuzi huo wa TCAA umekuja baada ya kuwepo kwa taarifa kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa CHADEMA, Tumaini Makene kuwa helikopta iliyokuwa itumiwe na Tundu Lissu pamoja na msafara wake wa kampeni jana Septemba 10, ilizuiliwa na mamlaka hiyo.

Buriani Mark Bomani
Wanafunzi zaidi ya 90,000 waomba mikopo