Waziri wa Madini Dotto Biteko amemvua madaraka Mwenyekiti wa Soko la Madini Chunya, pamoja na kuwasimamisha kazi wafanyakazi wengine watatu.
Biteko amefanya maamuzi hayo leo Desemba 14, 2020 alipotembelea soko hilo katika ziara yake anayoendelea nayo ikiwa ni siku chache tangu ateuliwe na kuapishwa kuitumikia Wizara hiyo kwa kile alichokieleza kuwa ni Mwenyekiti huyo kuwa mzembe hadi kusababisha madini kutoroshwa.
Aidha, Waziri Biteko pia amefuta leseni za wachimbaji watano ambao wamevunja taratibu mbalimbali na kuagiza mawakala na wanunuzi wa dhahabu watatu kukamatwa kwaajili ya kuchukuliwa hatua.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amemwagiza RPC kuwakamata wahusika wote na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria mara moja.