Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amemteuwa mwanaye, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, kuwa kamanda wa kikosi maalumu cha kumlinda rais, hatua inayoashiria uwezekano wa kuongezeka kwa ukandamizaji dhidi ya wapinzani.
Nchi hiyo inajiandaa kufanya uchaguzi mkuu Januari 14, 2021 ambapo tangazo kutoka makao makuu ya jeshi la Uganda, limesema Jenerali Muhoozi Kainerugaba atakiongoza kikosi hicho kijulikanacho kama SFC, chenye vifaa bora na mafunzo maalumu, ambacho aliwahi kukisimamia hadi alipoondolewa mwaka 2017 na kupewa majukumu ya mshauri wa rais.
Sakata la Mdee na wenzake laibuka upya
Wapinzani mara zote wamemtuhumu Rais Museveni kukipendelea kikosi hicho zaidi ya vikosi vingine vya jeshi la taifa hilo.
Rais Museveni, mwenye umri wa miaka 76 anawania muhula mwingine madarakani utakaouendeleza utawala wake hadi miaka 40.
Hata hivyo mpinzani wake mkuu katika uchaguzi ujao, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, amekabiliwa na ukandamizaji mkubwa kutoka katika vyombo vya usalama.