Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema daraja la Kigongo- Busisi limepewa jina la Rais John Magufuli ili aendelee kukumbukwa kutokana kazi aliyoifanya kwenye Utawala wake.
Majaliwa ameeleza hayo leo alipotembelea na kukagua ujenzi wa daraja hilo ulioanza mwaka huu 2020 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2024.
Daraja hilo linalojengwa na kampuni ya CCECC ya hapa nchini lina urefu wa Kilomita 3.2, litakuwa na nguzo 67 na litagharimu fedha Tsh. Bilioni 699.2.
Aidha, Waziri Mkuu amesema, ujenzi wa miradi mbalimbali ya kimkakati inayoendelea ina lengo la kurahisisha wananchi kufanya shughuli zao na amewataka Watanzania kupuuza kauli za baadhi ya watu kwamba Serikali inajali zaidi vitu badala ya kuleta Maendeleo ya watu.