Baraza la wawakilishi katika bunge la Marekani limepiga kura na kupitisha mashtaka ya kumvua madaraka Rais wa nchi hiyo Donald Trump, kufuatia mashtaka ya kuchochea vurugu na uvamizi wa majengo ya bunge wiki iliyopita.
Wabunge 10 wa chama cha Republic ni miongoni mwa waliopiga kura na Wademocrat dhidi ya Trump.
Trump amekuwa Rais wa kwanza katika historia ya Marekani kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye mara mbili.
Hata hivyo baraza la Seneti halitaanza mchakato wa kupitisha au kuzuia hatua hiyo ya baraza la wawakilishi kabla ya kuapishwa kwa Rais mteule Joe Biden Januari 20.
Endapo baraza la seneti litamkuta na hatia hata baada ya kuondoka madarakani, huenda atazuiwa kuwania urais tena katika uchaguzi ujao wa mwaka 2024.