Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema mwenendo wa nchi tajiri kujilimbikizia chanjo za Covid 19 na kuzisahahu nchi masikini kutapelekea kuongezeka kwa ugonjwa huo.
“Zaidi ya dozi milioni 39 za chanjo sasa zimo mikononi mwa takriban nchi 49 tajiri. Ni dozi 25 tu zimepelekwa katika nchi moja peke yake yenye uchumi wa chini, sio milioni 25, sio 25,000, bali ni dozi 25 tu,”amesema Mkurugenzi wa WHO wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wiki moja wa Bodi ya Utendaji ya WHO.
Tedros ametoa Rai kwa nchi wanachama wa WHO kuhakikisha chanjo zinazotolewa kwa kila taifa, ili kuondokana na mlipuko huo
Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO, idadi ya watu wanaougua ugonjwa wa COVID-19 ulimwenguni imepindukia milioni 93.8, na zaidi ya watu milioni 2.02 wamekufa kutokana na ugonjwa huo.