Mhubiri wa Kimataifa kutoka Nchini Nigeria, Temitope Balogun Joshua, maarufu TB Joshua amefariki Dunia jana jumamosi nchini humo akiwa na umri wa miaka 57
Taarifa iliyotolewa na kanisa lake la Scoan inaeleza kwamba TB Joshua alifariki muda mfupi baada ya kutoa huduma katika kanisa hilo lilipo jijini Lagos.
katika kipindi cha mahubiri cha Jumamosi Hayati Nabii TB Joshua akizungumza katika mkutano wa washirika kupitia Emmanuel TV alisema ‘kila jambo na wakati wake, kuna wakati wa kuja hapa kwa maombi na wakati wa kurudi nyumbani baada ya ibada’.”
Kupitia Ukurasa wake wa Instgram TB Joshua imeandikwa “Mungu amemuita nyumbani Nabii TB Joshua kwa mapenzi yake, nyakati zake za mwisho hapa duniani alizitumia katika huduma ya Mungu, hiki ndio kitu alichozaliwa kukifanya, alikiishi na kukifia,” inaeleza taarifa hiyo.
Itakumbukwa mwaka 2015 TB joshua aliitembelea Tanzania na kufanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa mgombea wa CCM, Hayati John Magufuli.
Tb Joshua, ndiye mwanzilishi wa Kanisa la Synagogue Church of All Nation (SCOAN) na Kituo cha Televisheni cha Emmanuel.