Nahodha na Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, John Raphael Bocco ameingia tena kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa klabu.

Bocco, ametangazwa kuwania tuzo hiyo sambamba na Viungo Washambuliaji Bernard Morisson kutoka nchini Ghana na Luis Miquissone kutoka nchini Msumbiji.

Kabla ya mchujo wa Kamati Maalumu ya tuzo hizo, imeeleza kuwa nyota hao walikuwa watano akiwamo Rally Bwalya kutoka Zambia na Pascal Wawa kutoka Ivory Coast.

Bernard Morrison ampaka sasa anaongoza kwa asilimia 67 ya Kura zinazoendelea kupigwa, akifuatiwa na Luis Miquissone mwenye asilimia 25.34 na John Bocco anashika nafasi ya tatu kwa kuwa na asilimia 7.18.

Bocco alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Simba SC mwezi Mei, kufuatia kuonesha kiwango kizuri tangu aliporejea kikosini na kufunga mabao mfululizo.

Bernard Morrison na Luis Miquissone wanapambana na Bocco katika tuzo ya mwezi Juni, baada ya kutoa msaada mkubwa katika kikosi cha Simba SC, kwenye michezo ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho ASFC.

Mbappe: Naomba mnisamehe
CECAFA U23 yasogezwa mbele