Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo, baada ya kukosa mkwaju wa penati, wakati wa mchezo wa UEFA Euro 2020 hatua ya 16 Bora dhidi ya Uswiz.

Mbappe alikosa mkwaju muhimu wa penati, baada ya timu hizo kwenda sare ya mabao 3-3 ndani ya dakika 120, na kuisababishia Ufaransa kutupwa nje ya michuano hiyo inayoendelea kwenye miji mbalimbali Barani Ulaya.

Mshambuliaji huyo wa klabu ya PSG alipiga mkwaju wa mwisho kwa Ufaransa ambao uliokolewa na mlinda mlango wa Uswiz Yann Sommer.

“Naomba samahani kwa kukosa Penati. Nilihitaji kuisaidia timu lakini nilikosa Penati. Kwa bahati mbaya nimeingia katika shimo la mpira wa miguu ninaoupenda sana, Kuwa na amani kwangu itakuwa kazi”

“Nafahamu mashabiki mmehuzunishwa, lakini napenda kuwashukuru kwa kutusapoti, na siku zote mmekuwa mkituamini. Kitu kikubwa cha msingi ni kujiandaa vizuri na michuano mikubwa inayokuja,” amesema Kylian Mbappe.

Baada ya kuiondoa Ufaransa kwa penati 5-4 , kikosi cha Uswiz kimetinga hatua ya Robo Fainali na kitacheza dhidi ya hispania.

Deschamps aikingia kifua Ufaransa
Morrison awatimulia vumbi Bocco, Muquissone