Kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ya kupewa muda kuhusu suala la katiba mpya ili aendelee na taratibu a kujenga uchumi wa nchi kwanza utakapokaa sawa ndipo atageukia mambo mengine ikiwemo swala la katiba.
Wakizungumza na Dar24Media kwa nyakati tofauti wananchi hao wamebaki njia panda kwa kuona kauli hiyo inaweza ikawa ni kauli sahihi au pia isiwe ni kauli sahihi, hata hivyo wamesema kuwa kama Rais samia ananshughulikia suala la uchumi inamaana anatumia katiba ile ile ya zamani katika utekelezaji.
Aidha wamesema kuwa watanzania wengi hawana uelewa wa katiba hata ya zamani hali inanyopelekea hata kama ikifanyiwa mabadiliko haitakuwa rahisi kwa mwananchi kuelewa mabadiliko yaliyofanyika endapo katiba mpya ikitoka.
Hali kadhalika baadhi ya wananchi pia wamesema ni sahihi kwa Rais kuanza na Uchumi kwasababu mchakato wa katiba unachelewesha maendeleo na pia ni mchakato ambao unahitaji hela itumike ili kukamili.
Wananchi hao wameongeza kuwa kila mmoja anautendaji wake katika kazi na misimamo yake hivyo ni vema kupewa muda.
Wameishauri serikali kuunda kamati itakayoweka mikakati ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na suala la katiba.