Kocha Mkuu wa Timu za taifa za Wanawake Bakari Nyundo Shime, ametaja kikosi cha timu ya taifa ya wakubwa (Twiga Stars), kitakachoingia kambini Julai 03, jijini Dar es salaam.

Shime ametaja kikosi hicho, huku akiwaacha wachezaji wa Simba Queens, ambao wanajiandaa na Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Mashariki na Kati(CECAFA Women’s Champions League).

Michuano hiyo imepangwa kuanza baadae mwezi huu nchini Kenya, hivyo Kocha Shime ameona ni bora akatoa nafasi kwa wachezaji wa Simba Queens kuendelea na maandalizi ya ushiriki wa CECAFA Women’s Champions League.
Twiga Stars itaingai Kambini ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na michuano mbalimbali kwa siku za usoni, ambapo utaratibu huo hufanywa mara kwa mara na Kocha Shime.

Kikosi cha Twiga Stars kilichotajwa na Kocha huyo mzawa.

Fiston Mayele: Natamani kucheza Tanzania
Tanzania ya pili Afrika katika usalama wa kimtandao