Afisa Mhamasishaji wa Young Africans Antonio Nugaz ameonesha wasiwasi kuelekea mchezo wa kesho Jumamosi (Julai 03), kwa kuitaka Simba SC kuacha ‘JANJA JANJA’.

Nugaz amesema mchezo wa kesho unapaswa kubeba uungwana wa hali ya juu ili kurpuka malalamiko dhidi ya mwamuzi Emmanuel Mwandembwa kutoka jijini Arusha.

Amesema walichokifanya Simba SC kwenye mchezo wao dhidi ya Azam FC na kupelekea kupata bao la ushindi lilifungwa na Luis Miquissone, hakipaswi kufanywa kwenye mchezo wa kesho unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki kila kona ya nchi.

“Tucheze mprira wa kweli na siyo ujanja ujanja, refa anaongea na wachezaji nyie mnaanzisha mpira, ile Kama waliyowaanzishia wenzetu wala siyo”

“Kwa sasa najiamini kuliko kipindi chochote, Kwanza Kikosi Cha kutufunga wanacho? Majigambo tu wale, wenyewe waje tu uwanjani mpira ni dakika 90 zitaenda kuamua nani mwenye Kikosi kipana na nani mwenye Kikosi chenye muunganiko mzuri,” Amesema Nugas.

Simba SC inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 73, inahitaji alama tatu kujihakikishia ubingwa msimu huu.

Young Africans yenye alama 67, inashika nafasi ya pili kwenye msimamo, inatakiwa kushinda mchezo wa kesho Jumamosi ili kuendeleza Presha ya ubingwa msimu huu dhidi ya Mabingwa Watetezi Simba SC.

Timu hizo kongwe zimesalia kwenye mbio za ubingwa, kufuatia Azam FC kufikisha alama 64 huku ikisaliwa na michezo miwili mkononi.

EndapoAzam FC itashinda michezo yake dhidi Simba SC na Ruvu Shooting, itafikisha alama 70 ambazo hazitawatosha kufanikisha kuwa mabingwa msimu huu.

Lamine Moro: Sijui nimekosea wapi
vibaka, majambazi watafute kazi nyingine - Kamanda Kyando